:: NYUMBANI :: WASILIANA NASI   :: CONTACT US :: HOME
SDA Tanzania (logo)
Utambulisho
Habari
Miradi iliyopo
Hifadhi ya Habari
Links
Liikunnan Kehitysyhteistyö LiiKe ry

MIRADI ILIYOPO

SDA inatekeleza shughuli zake za mwaka kupitia miradi yake tofauti. Kwa sasa kuna miradi miwili inayotumika.

ELIMU KUPITIA MICHEZO

Lengo la mradi huu ni kutumia michezo kama chombo cha kuvutia wanafunzi shuleni. Inajumuisha uandaaji wa mashindano katika shule, Ufundishaji wa michezo mipya, uboreshaji wa viwanja vya michezo pamoja na uendeshaji seminar mbalimbali za michezo kwa walimu wa michezo. Mradi huu unafadhiliwa na wizara mambo ya nje ya Ufini mpaka mwaka 2006.

RAFIKI KATIKA MICHEZO

Katika mradi huu wa pamoja kati ya SDA pamoja na LiiKe, kwa pamoja asasi za michezo 41 zinasaidia baadhi ya shule za msingi zilizopo mkoani Mtwara kwa kuchangia Euro 250 kwa mwaka. Asasi hizi zinakusanya vifaa vya michezo kamo Jezi, mipira na viatu vya michezo kwa ajili ya kusambaza kwenye shule. Shule zinawajibika kuandika ripoti kwa asasi rafiki iliyo wapatia vifaa ili kuwajulisha maendeleo yao katika michezo.

Introduction
News
Projects
Material bank
Links
United Nation’s International Year of Sport and Physical Education 2005